} });
 

 

Mwimbaji wa Marekani Robert Kelly maarufu R Kelly amekutwa na hatia ya kutumia hadhi yake ya kuwa nyota kuendesha mpango wa kuwadhulumu kingono wanawake na watoto kwa zaidi ya miongo miwili.

Majaji waliokua wakisikiliza kesi hiyo wamesema R Kelly amekutwa na kosa la kuwa kiongozi wa mpango uliyowavutia wanawake na watoto na hatimaye kuwanyanyasa kingono.

Mwimbaji huyo amegundulika kuwasafirisha wanawake kati ya majimbo tofauti ya Marekani na kuandaa filamu ya ponografia ya watoto.

Walalamikaji 11, ikiwemo wanawake tisa na wanaume wawili, wametumia wiki sita kuelezea udhalilishaji wa kingono na ghasia walizokumbana nazo mikononi mwake.

Katika mkutano na wanahabari nje ya mahakama siku ya Jumatatu, mwendesha mashtaka Jacquelyn Kasulis amesema jaji ametuma ujumbe mkali kwa wanaume wengine wenye uwezo kama Kelly.

“Haijalishi itachukua muda gani, mkono mrefu wa sheria utakunasa,”alisema Bi. Kasulis.

Baada ya siku mbili ya majadiliano, jaji aliekua akisikiliza kesi hiyo amesema R Kelly ana hatia katika mashtaka yote yaliyokuwa anakabiliwa nayo na huenda akafungwa maisha.

Nyaraka za kisheria pia zilifichua mateso ya kiakili ambayo Kelly aliwafanyia wanawake hao na hawakuruhusiwa kula au kwenda msalani bila idhini yake huku akiamua nguo walizovaaa na kuwafanya wamuite “Daddy”.

Uamuzi huo unakuja miaka 13 baada ya R Kelly kufutiwa mashtaka ya ponografia ya watoto baada ya kushtakiwa katika jimbo la Illinois.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top