} });
 


Mbunge wa Jimbo la Ngorongoro wilayani Ngorongoro mkoani Arusha ambaye pia ni Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji, William Ole Nasha amefariki dunia Septemba 27, 2021 nyumbani kwake jijini Dodoma.

 

Kifo cha Mheshimiwa Ole Nasha kimethibitishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan.

 

“Nasikitika kuwajulisha kuwa aliyekuwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwekezaji Mhe. William Tate Ole Nasha amefariki dunia Jijini Dodoma. Natoa pole kwa Spika Mhe. Job Ndugai, Wabunge, Familia na Wananchi wa Ngorongoro. Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amina.”- Rais Samia.


Rais Samia apokea kwa masikitiko taarifa ya kifo cha Ole Nasha.soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top