
Rais wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi ameivunja bodi
ya ushauri ya kudhibiti vileo Zanzibar.
Taarifa
iliyotolewa kwa vyombo vya habari na kusainiwa na Katibu wa Baraza la Mapinduzi
na Katibu Mkuu Kiongozi, Zena Said imesema hatua hiyo ni kuanzia Jumanne
Septemba 7, 2021.
Bodi hiyo
ilikuwa chini ya usimamizi wa Ofisi Rais, Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na
Idara Maalumu za SMZ.
Pia, Rais Mwinyi ametengua uteuzi wa Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Viwango ya Zanzibar (ZBS), Rahima Ali Bakari.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment