} });
 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Sulihiu Hassan amesema kuwa amefanya mabadiliko ya muundo wa Wizara mbili ya Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na michezo kubaki Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo na Habari kuipeleka kwenye Wizara ya Habari.

Rais Samia amefanya mabadiliko hayo ili kuifanya Wizara ya Habari Mawasiliano na Teknolojia ya Habari kutimia, kitu ambacho ilikuwa ni ndoto ya muda mrefu kwa watu wa sekta ya habari.

Ameyasema hayo leo Septemba 13, 2021 wakati wa hafla ya kuwapisha viongozi mbalimbali walioteuliwa, huku akielezea sababu zilizomfanya kufanya mabadiliko hayo ikiwa ni pamoja na kutoa msukumo mkubwa kwa Wizara ya Sanaa Utamaduni na Michezo kwasababu ilikuwa inamezwa kwa kiasi kikubwa na iadara ya Habari.

“Nimeona niiiachie ionekane kwa uwazi zaidi kwasababu Sanaa, Utamaduni ni Michezo ni ajira kwa vijana wetu wengi sana lakini pia ni utalii,” Amesema Rais Samia.

Hata hivyo Rais Samia amesema kuwa kwa kuipa nafasi Sanaa na Utamaduni itasaidia pia kukuza jina la Nchi.

Sambamba na hayo yote pia Rais Samia amesema amevunja mwiko/ tafsiri mbaya ya muda mrefu kuwa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa huongozwa na mwanaume, ambapo amesema kazi ya Waziri sio kupiga mitutu bali kuhakikisha kila jambo liko kwenye mstari wake.

“Kipindi cha SADC alikuwa anasimamia vema hivyo atakwenda kutusaidia,” Amesema Rais Samia.

Aidha Rais Samia amewahasa viongozi hao walioteuliwa kufanya kazi kwa bidii kwani anachotaka ni kuona matokeo kwa haraka lakini pia amewahasa kufanya mabadiliko pale wanapodhani panahitaji mabadiliko.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top