
New Delhi,
India (AFP). Saluni nchini India imeamriwa kumlipa mwanamitindo zaidi
ya dola 271,000 za Kimarekani (sawa na takriban Sh627.4 milioni za Kitanzania)
kutokana na kumnyoa nywele kinyume cha utashi wake, kitu ambacho amedai
kilimsababishia "matatizo ya kiakili".
Aashna
Roy alienda saluni hiyo iliyo juu ya hoteli moja jijini New Delhi mwaka 2018 na
akataka kinyozi apunguze nywele kwa urefu wa sentimita 10, kwa mujibu wa hukumu
iliyotolewa na mahakama ya wateja ya jiji.
"Hata
hivyo, kwa mshangao mkubwa wa mlalamikaji, kinyozi huyo alinyoa nywele zake
zote akiacha zikiwa na urefu wa sentimeta nne tu na hivyo kugusa mabega yake
kwa shida," inasema hukumu hiyo.
Mahakama
hiyo imeamua kuwa kutokana na ukweli kuwa Roy alishajijenga kama mwanamitindo
na kuchukuliwa kwa ajili ya matangazo ya bidhaa za nywele, ukataji huo wa
nywele ulimsababishia "matatizo makubwa ya kiakili na mfadhaiko".
"Hakuna
shaka kuwa wanawake wako makini sana na waangalifu kwa nywele zao,"
inasema hukumu hiyo iliyotolewa na Kamisheni ya Kurekebisha Mizozo ya Walaji.
"Wanatumia
fedha nyingi kuziweka nywele katika hali nzuri. Nywele pia zinagusa hisia
zao," iliongeza.
"Kwa
hiyo alikosa kazi alizozitarajia na kuingia hasara kubwa ambayo ilibadilisha
kabisa hali yake ya maisha na kuzima ndoto yake ya kuwa mwanamitindo wa viwango
vya juu."
Mahakama imeiambia saluni hiyo, ambayo inaweza kukata rufaa kupinga hukumu hiyo, ilipe rupia 20 milioni za India ndani ya wiki nane tangu kutoka kwa hukumu hiyo.
Post a Comment