
Bodi ya Utendaji ya
Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF) imekubali kuipa Tanzania dola za Marekani
milioni 567.25 (Sh1.3 trilioni) ambazo ni msaada wa dharura kwa ajili ya
kushughulikia janga la Uviko-19.
Mlipuko wa
ugonjwa huo nchini umesababisha kuanguka kwa sekta ya utalii na kuongeza hitaji
la ufadhili mkubwa ili kukabiliana na athari za kiafya na kiuchumi za janga
hilo.
IMF
iliidhinisha msaada huo wa dharura wa kifedha chini ya kituo cha mikopo ya
haraka kwa lengo la kuunga mkono juhudi za mamlaka katika kukabiliana na janga
hilo kwa kushughulikia gharama za haraka za kiafya, kibinadamu na za kiuchumi.
Mtazamo wa
uchumi wa Tanzania umedorora kutokana na athari za janga la Uviko-19 pamoja na
kuanguka kwa utalii baada ya vizuizi vya kusafiri, uchumi unaripotiwa kupungua
kwa ukuaji wa asilimia 4.8 mwaka 2020, na ukuaji unatarajiwa kubaki chini kwa
mwaka 2021.
Tanzania
inahitaji fedha za haraka karibu asilimia 1.5 ya Pato la Taifa kama mamlaka
kutekeleza mpango mpana wa kupunguza athari za janga hilo na kuhifadhi utulivu
wa uchumi mkuu mbele ya wimbi la Uviko-19.
Taarifa hiyo
imeeleza kuwa Serikali imeonyesha nia kwa kufuata sera za uchumi zinazofaa
kushughulikia athari za janga hilo na kujitolea kuimarisha uratibu na uwazi ili
kuhakikisha kuwa rasilimali hizo zinatumika katika kupambana na janga hilo.
Naibu Mkurugenzi
Mtendaji na Mwenyekiti wa Bodi ya Utendaji, Bo Li, ametoa taarifa ifuatayo:
"Janga
la Covid-19 limeathiri mtazamo wa uchumi mkuu wa Tanzania katika afya na ustawi
wa idadi ya watu.
“Ukuaji wa
uchumi umepungua kuanzia mwaka 2020 na unatarajiwa kubaki chini kwa mwaka 2021,
kuongezeka kwa umasikini na kuathiri ajira. Hatari ya Tanzania kuendelea kuwa
na deni kubwa nje ya nchi imeongezeka hadi wastani, haswa kutokana na athari ya
janga hilo kwa fedha zilizopatikana kupitia utalii.
"Mamlaka inatekeleza mpango kamili wa kukabiliana na janga hilo kijamii na kiuchumi, Tanzania inahitaji msaada wa haraka wa kifedha kutekeleza mpango huu na kuiepusha mdororo wa kiuchumi,” amesema Bo Li.
Post a Comment