} });
 


Watu wapatao 41 wamefariki baada ya moto kutokea katika gereza katika gereza la Indonesia lililopo pembezoni mwa Mji Mkuu wa Jakarta.

Moto huo ulitokea katika gereza la Tangerang wakati wafungwa wengi wakiwa wamelala.

Kulikuwa na wafungwa 122 katika gereza C ambalo liliathiriwa na moto. Ila gereza lote lina wafungwa 2,000 idadi iliyozidi kiwango cha gereza hilo ambacho ni watu 600.

Wafungwa hao wengi walikuwa wanashikiliwa kwa makosa ya kujihusisha na dawa za kulevya. Watu kadhaa wanadaiwa kujeruiwa wengine wakiwa kitengo cha mahututi.

Hitilafu ya umeme inadaiwa kuwa chanzo cha moto huo, amesema msemaji wa gereza hilo ingawa amesema pia uchunguzi zaidi unafanyika.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top