} });
 

 

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mbeya imemhukumu mkazi wa Kata Mjele, Wilaya ya Mbeya, Mateso Wilson (34) kunyongwa hadi kufa baada ya kupatikana na hatia ya kumuua na kunyofoa viungo vya mkewe. 

Mateso alidaiwa kumuua mkewe Zaina Mela na kunyofoa viungo vyake  yakiwemo maziwa na masikio. 

Hakimu Mkazi Mfawidhi, Zawadi Laizer ametoa hukumu jana Jumatano Oktoba 20, 2021 baada ya mahakama kuridhika kuwa ushahidi wa upande wa Jamhuri haukuacha shaka yoyote. 

Ilielezwa  mahakamani hapo kuwa mnamo  April  22 , mwaka 2017  mshtakiwa Wilson alishirikiana  kufanya mauaji hayo na wenzake wawili  kwa lengo la kupeleka kwa mganga wa kienyeji ili wapate utajiri wa kudumu.

Wenzake walioshirikiana nao katika mauaji hayo hawajakatwa. 

Hakimu Laizer amesema   mahakama imezingatia  maelezo ya pande mbili  na ushauri wazee wa mahakama kabla ya kufikia uamuzi huo. 

Mshtakiwa ambaye alikuwa akiwakilishwa na wakili wa kujitegemea, Hilda Mbele  aliiomba mahakama kumpunguzie adhabu.

Hata hivyo, upande wa Jamhuri ukiongozwa na Wakili wa Serikali,  Davice Msanga aliomba mahakama kutoa adhabu kali ili iwe fundisho kwa wengine.

Hakimu Laizer ameeleza mahakama hiyo  kuwa mshtakiwa anahukumiwa kunyogwa hadi kufa  ili iwe fundisho kwa watu wengine ambao wanatafuta mali kinyume cha utaratibu.

Kisheria, ni Mahakama Kuu pekee ndiyo yenye mamlaka ya kusikiliza na kuamua kesi za mauaji. Hata hivyo Mahakama hiyo inamamlaka ya kutanua wigo wa mamlaka yake na kuziruhusu Mahakama za chini kusikiliza kesi za aina hiyo pale kunapokuwa na mahitaji.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 1. The blog are the best that is extremely useful to keep.
  I can share the ideas of the future as this is really what I was looking for,
  I am very comfortable and pleased to come here. Thank you very much!
  wordpress Casino
  ufa88kh.blogspot Casino
  youtube Casino
  កាស៊ីណូអនឡាញ CASINO ONLINE

  ReplyDelete

 
Top