} });
 

 

Kijana Michael Paul (18), mkazi wa Luanzari, Kata ya Ng’ambo, Manispaa ya Tabora, amekutwa amefariki dunia kwa kujinyonga na shuka chumbani kwake na kuacha ujumbe akimuomba msamaha mama yake na kusema maisha ndiyo chanzo cha yeye kujiuwa hivyo amzike.

 

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora ACP Richard Abwao, amesema kuwa tukio hilo limetokea Oktoba 24, 2021, na taarifa za kujinyonga kwa kijana huyo zilitolewa na dada wa marehemu aitwaye Jane Paul.

 

Kamanda Abwao amesema marehemu kabla ya kujinyonga aliacha ujumbe wa maandishi uliosomeka; “Mama naomba unisamehe ni maisha tu yamenifanya nijiue mnizike.”

 

Chanzo cha tukio kimetajwa kuwa ni msongo wa mawazo, na mbinu aliyotumia ni kujifungia chumbani kisha kujitundika juu ya kenchi kwa kutumia shuka.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top