} });
 

 

NA FAUSTINE GIMU GALAFONI - DODOMA

WAZIRI  wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto,Dk Dorothy Gwajima  amesema kuwa bima binafsi zote za matibabu  zitajumuishwa wakati wa kujadili sheria  ya Huduma ya Bima ya Afya kwa wote ambayo iitajadiliwa na Bunge la Novemba  mwaka huu.

 

Dk Gwqjima ametoa kauli hiyo Jijini Dodoma  wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya[ NHIF] ambapo amesema  Serikali imejipanga kuhakikisha kila Mtanzania anapata matibabu kwa urahisi, kupitia sheria ya huduma za bima ya afya  kwa wote  na Sheria hiyo itajadiliwa na wabunge Ili ipate maoni na ridhaa kuelekea kuwa sheria.

 

Amebainisha kuwa Sheria itajadiliwa kwqni kuna mifuko ya Bima ya Afya ikiwemo Mifuko wa NHIF, Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF), Bima zote binafsi zitatazamwa kwenye sheria, wote watajumuishwa na kutazamwa Ili kuwe na tija kwa wote.

Mwenyekiti wa kamati ya  kudumu ya Bunge ya huduma za Jamii Stanslaus Nyongo amesema wataendelea kuwa tayari kutoa ushirikiano na kuhakikisha wanafanikisha yale yote waliyopangwa huku Mwenyekiti  mstaafu  Bodi ya Wakurungenzi NHIF ambaye pia ni Spika Mstaafu Anne Makinda akisisitiza umuhimu wa bima.

Mkurugenzi Mkuu wa NHIF, Benard Konga amezungumzia mafanikio ya mfuko huo ambapo   kuna vituo 8,000 Nchini  vinatumia mfumo wa TEHAMA huku mwenyekiti wa Bodi wa mfuko huo huku mwenyekiti bodi ya Wakurugenzi wa NHIF Juma Muhimbi akitoa shukrani kwa waliofanikisha katika zoezi hilo

Katika kilele hicho cha Miaka 20 za NHIF zilitolewa tuzo mbalimbali kwa viongozi wastaafu Pamoja na taasisi mbalimbali zizokuwa mstari wa mbele katika kuhamasisha jamii ikiwemo Umoja wa Klabu ya Waandishi wa Habari Tanzania.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top