} });
 


Mkazi wa kijiji cha Busanda kata ya Busanda wilayani Geita Unice Kulwa(25) na wanawe wawili wamepoteza maisha baada ya kukosa hewa kutokana na kuingiza  jiko la mkaa alilokuwa akipikia maharage kwenye nyumba waliyolala. 

Mbali na vifo hivyo pia baba wa familia hiyo Kulwa Kamili amenusurika kifo na amelazwa kwenye kituo cha afya Katoro akiendelea kupatiwa matibabu. 

Mkuu wa Wilaya ya Geita, Wilson Shimo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema limetokea usiku wa kuamkia Oktoba 3, 2021 katika kitongoji cha Shilungule kijiji cha Busanda wilayani humo.

Aliwataja watoto waliopoteza maisha kuwa ni Kamuli Kulwa(5) na Jenipha Kulwa (3)

Akielezea tukio hilo Ofisa mtendaji wa Kata ya Busanda Victoria Mapunda amesema mama huyo baada ya kumaliza kupika chakula cha usiku aliinjika maharage jikoni na kwenda kulala na saa tisa usiku mmoja wa majirani alihisi hali ya tofauti na  na alipotoka nje alikutana na hali ya tofauti. 

Amesema jirani huyo aliwaamsha majirani zake bila mafanikio na kuamua kugonga kwa jirani mwingine ambaye waliamua kuvunja mlango na kuingia ndani na kuwakuta wazazi hao na watoto hawajitambui huku nyumba ikiwa na joto kali. 

“Majirani waliwakimbiza Zahanati ya Shilungule na walipofika mama na wanawe wawili walifariki huku baba alipewa huduma ya kwanza na kupelekwa kituo cha afya Kaqtoro na hali yake inaendelea vizuri”amesema Victoria. 

Katika hatua nyingine Mkuu wa Wilaya amewataka wananchi kuchukua tahadhari na kuacha tabia ya kuingiza jiko ndani huku wao wakiwa wamelala na kuchukua tahadhari za majanga mengine hasa wakati huu wa msimu wa mvua ikiwa ni kuhakikisha vyoo wanavyotumia ni imara. 

“Tunaelekea msimu wa mvua ,tuchukue tahadhari,vyoo viwe salama ,funikeni visima vya asili,mashimo ya mchanga na mito tuvuke kwa tahadhari”amesema Shimo

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top