Waziri wa
Mkuu, Kassim Majaliwa amesema zoezi la chanjo ya Uviko-19 limefikia zaidi ya
asilimia 80 na zilizobakia mikoani hivi sasa ni chache.
Jumla ya chanjo milioni 1.058 zilizopokelewa nchini kutoka nchini Marekani
Julai 24, 2021 na uchanjaji ulizinduliwa rasmi Julai 29, 2021 na Rais Samia
Suluhu Hassan.
Kauli hiyo imekuja baada ya Serikali kuanzisha kampeni maalum ya kuhamasisha
uchanjaji wa chanjo hiyo katika maeneo mbalimbali ikiwemo makanisani na kwenye
mikusanyiko ya watu.
Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatatu Oktoba 4 2021), wakati akifungua kongamano
la tano la uwezeshaji lililoandaliwa na Baraza la Taifa la Uwezeshaji Wananchi
Kiuchumi (Neec).
“Tunalo zoezi la uchanjaji. Namshukuru Mungu tumefikia asilimia 80 na kitu
huko, tumebaki na chanjo chache sana kwenye mikoa hiyo. Kila mmoja awahi huko
na kama kuna mahitaji tutaleta nyingine malengo ni afya,”amesema.
Amesema suala la chanjo sio lazima lakini ni muhimu kwaasababu linasaidia
kuongeza virutubisho mwilini na iwapo mtu atapata hawezi kuwa mwepesi kama vile
mtu ambaye hajachanjwa kabisa.
Amewaagiza wakuu wa mikoa kutoa elimu na kuhamasisha kuhusu umuhimu wa kuchanja chanjo hiyo.
Post a Comment