Agnes Charles, mtoto mwenye umri
wa miaka mitatu amekufa baada ya kuangukiwa na matofali akiwa amelala
baada ya nyumba kubomoka wakati tembo wakitaka kuingia ndani kula viazi
vikavu vilivyokuwa vimehifadhiwa katika nyumba hiyo.
Kamanda wa
Polisi Mkoa wa Simiyu, Richard Abwao amewaeleza waandishi wa habari kuwa
tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia Septemba 29, 2021 saa mbili
usiku katika kijiji cha Mwanzagamba wilayani Meatu.
Abwao amesema tembo wawili walivamia makazi na kuvunja nyumba ambayo mtoto alikuwa amelala pia palihifadhiwa chakula ambacho tembo walikuwa wanakitafuta.
Ameeleza
kuwa mama wa mtoto huyo alikimbia na watoto wake wengine wawili aliokuwa
nao nje wakati tembo wanavamia, "baada ya tembo kuondoka ndipo
alirudi kwa ajili ya kumwokoa mwanaye na kumpeleka katika hospitali ya wilaya
ya Meatu ambapo aligundulika kuwa tayari amefariki."
Post a Comment