
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Ramadhani Kingai akisoma maelezo ya mshtakiwa wa pili katika kesi ya uhujumu uchumi, Adam Kasekwa amesema mtuhumiwa huyo alisema Freeman Mbowe alipanga kumdhuru aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai Ole Sabaya.
Katika ushahidi alioutoa jana, Oktoba 26, 2021 katika Mahakama Kuu Divisheni ya Makosa ya Rushwa na Uhujumu Uchumi, Kingai amesoma maelezo ya mtuhumiwa huyo kwamba Mbowe alisema Sabaya anahatarisha nafasi yake ya kuendelea kuwa mbunge wa Hai.
Ifuatayo ni sehemu ya maelezo ya
mshtakiwa Adamu kama yalivyosomwa na RPC Kingai:
“Mbowe alituelekeza tufuatilie nyendo zake na tumdhuru kwa spray ya sumu. Ling'wenya alifuatilia mtu wa kupata sumu. Tarehe 27 tulirudi Dar na magari mawili pamoja na Mbowe na mlinzi wake.
“Baada ya kufika Dar tulifikishwa Mikocheni mimi na Ling'wenya tulipewa Sh200,000 tujiandae. Baadaye tulipewa nauli turudi Moshi. Agosti Mosi saa 11 alfajiri Mbowe alituita akasema tutekeleze maelekezo ya kumdhuru Sabaya.
“Akituonesha
picha ya Sabaya na maeneo anauyopenda kutembelea. Alituelekeza baada ya kazi ya
Sabaya turudi Dar kutekeleza kazi nyingine nyeti kulipua vituo vya mafuta na
kushinikiza maandamano ili Serikaki ionekane imeshindwa maana inatuchukia sisi
wapinzani.
“Yeye
aliondoka kurudi Dar sisi tukabaki kutekeleza kumdhuru Sabaya Tarehe 3 Atosti
tulienda eneo la Rao Madukani kwa dada yake Ling'wenya ili kubana matumizi
maana Mheshimiwa alituachia Sh150,000
“Tulikamatwa
na askari tukituhumiwa kukutwa na dawa za kulevya na kupanga njama za ugaidi.
Tuhuma hizo ni za kweli na pia kukutwa na silaha ni za kweli na nilikutwa na
simu yangu ya Itel.
“Nilisaini
hati ya kuchukuliwa mali na askari nao wakasaini. Nikachukuliwa kwenda Central
Moshi. Uthibitisho haya maelezo ni ya kweli kwa saini.
“Muda
wa kumaliza kuandika maelezo hayo ilkiuwa ni saa 3"
Wakili
wa Serikali Mwandamizi SSA Kidando alimtaka ACP Kingai aelezee
alichoelezwa na mshtakiwa huyo wa pili Adamu.
ACP
Kingai :Alikiri kukutana na wenzake kwa ajili kwenda kwa Mbowe, alikiri kupewa
nauli kwenda Moshi kukutana na Mbowe, alikiri kuwepo Moshi tarehe 24 -26 Julai
2020, alikiri kuwepo yeye na wenzake wawili akiwemo Ling'wenya na mtu mwingine.
“Alikiri
tarehe 25 usiku kufanya mkutano yeye na Ling'wenya, Moses Lujenje maarufu
Kakobe, Hassan Bwire na Freeman Mbowe"
SSA
Kidando: Nini kiliendelea?
ACP
Kingai : Alikiri kwenye mkutano alielekezwa na Mbowe kumdhuru DC Sabaya kwa
njia yoyote ile.
SSA
Kidando: Kitu gani kingine alikueleza?
ACP
Kingai: Shahidi pia alikiri kupewa pesa na Mbowe Sh150,000 kukidhi
mahitaji hapo Moshi, alikiri Agosti Mosi 2020 alfajiri Mbowe aliwaita tena na
kuwapa maelekezo, kwamba wahakikishe wanayafanyia kazi.
“Kumdhuru
Sabaya na ili wawe na uhakika Mbowe aliwaonyesha picha ya Sabaya kupitia simu
yake, aliwalekeza wamalize kazi hiyo ya Moshi halafu warudi Dar kufanya kazi
nyingine nyeti.
“Alitaja kazi hiyo kwamba walipanga wakalipue vituo vya mafuta, lakini pia kufanya vurugu kwenye masoko na maeno ya watu wengi”.
Post a Comment