Huduma za mitandao ya
kijamii ya Facebook, WhatsApp na Instagram zimerejea baada ya
kutopatikana kwa saa nane.
Kupitia
taarifa ya Facebook imeeleza kuwa sababu ya kutoweka kwa mitandao hiyo ni
mifumo kutofanya kazi.
Huduma zote
tatu zinamilikiwa na Facebook na hazikuweza kupatikana kwenye wavuti au kwenye
programu za simu za mkononi.
Taarifa
zinaeleza kuwa kukatika kwa huduma hizo ni hitilafu kubwa zaidi kuwahi kutokea.
Katika
taarifa hiyo iliyotumwa usiku wa kuamkia leo Jumanne Oktoba 5,2021 imesema
mabadiliko mabaya ya usanifu yaliathiri zana na mifumo ya ndani ya kampuni
hiyo.
Facebook ilituma ujumbe wa kuomba radhi kwa walioathirika kutokana na kutokupatikana kwa huduma zake za mitandao ya kijamii.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment