} });
 


Album mpya ya rapa machachari kutoka nchini Marekani Kanye Omar West  aliyoibatiza jina la marehemu mama yake mzazi ‘DONDA’ inaendelea kufanya vizuri tangu imeachiwa rasmi Aug 29, 2021, kwa mujibu wa ripoti kutoka Spotify album hiyo imefanikiwa kufikisha jumla ya wasikilizaji 1 Bilioni kwenye mtandao huo maarufu Duniani.

Kwanini tunaendelea kuona kustawi wa maendeleo ya mauzo ya album hiyo?

Kanye anatajwa kama mmoja wa wasanii wenye uwezo mkubwa sana kifikra hasa linapokuja swala la umakini katika biashara zake ikiwamo umahiri katika kuweka mikakati madhubuti ya kibiashara, watu wengi siku za hivi karibuni wame endelea kushangazwa na mwenendo wa mtindo wa maisha yake hasa mavazi na muonekano wa msanii huyo mwenye kuzua matukio mapya kila kukicha huku akiacha mijadala katika kila pembe ya Dunia kupitia mitandao ya kijamii ambayo ndio sehemu kubwa wanako patikana wateja wa muziki na bidhaa zake.

Unadhani ni kwanini Kanye West haishi vituko?

Wakati sisi tunafurahia au kuushangazwa na mtindo wa maisha ya msanii huyo huku kila mmoja akijiuliza maswali ya kuwa pengine Kanye si mzima kiakili, unaamiwa muda huo yeye anahesabu kuwa kumzungumiza kwako na kutenga muda wako kumfuatilia japo kwa sekunde 60 tu, tayari katimiza lengo kwa kuwa kila anachokifanya na kikawa gumzo Duniani huwa hakitokei kwa bahati mbaya.

Kitu cha tofauti kwenye maisha ya Kanye west ukilinganisha na wasanii wengine kwenye kazi, yeye ameamua kuchagua njia ya kuendelea kufanya promotion ya kazi zake kabla ya kutoa na huendelea kuipambania hata baada ya kazi hiyo kuwa sokoni, zoezi hili kidogo kwa baadhi ya wasanii si rafiki kwao, wengi huthubutu kuweka nguvu kubwa kabla na mwanzo pekee ila mbeleni huachilia mbali.

Ukiachana na ushindani uliopo sokoni na fujo za mashabiki wenye kuoanisha namba za nani kasikilizwa zaidi na nani yupo chini kidogo, Nani kapanda na kushuka chati, ila  kwa sasa unaambiwa tegemea maajabu zaidi kwenye kila anachokifanya msanii huyo kutokana na miakakti mikubwa aliyo nayo katika kila alifanyalo.

Kanye west siku za hivi karibuni alitangaza kubadilisha jina lake rasmi kutoka Kanye Omar West mpaka kuwa ‘YE’.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top