} });
 

 

NA FAUSTINE GIMU GALAFONI - DODOMA

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema mabalozi wanaoteuliwa kuiwakilisha Tanzania nje ya nchi wanapaswa kutanguliza maslahi ya Taifa katika utekelezaji wa majukumu yao.

 

Amesema kuwa mabalozi hao wanapaswa kutekeleza falsafa ya Mheshimiwa Rais Samia ya kuona kazi zilizoratibiwa zinaendelea kutekelezwa kwa uadilifu mkubwa na uaminifu ili ziweze kutoa matokeo chanya katika kila kazi zinazofanyika.

 

Waziri Mkuu ametoa wito huo leo (Jumapili, Oktoba 3, 2021) ofisini kwake Mlimwa jijini Dodoma wakati alipokutana na mabalozi saba watakaoiwakilisha Tanzania katika nchi za Uturuki, Sweden, Rwanda, India, Ethiopia, Uswisi na Jamhuri ya Korea.

 

Waziri Mkuu amesema mabalozi hao wana jukumu la kukuza uchumi wa Tanzania kupitia diplomasia ya uchumi.

 

Amesema ili Tanzania iweze kupaa zaidi kiuchumi, inapaswa kukuza sekta ya viwanda hatua ambayo itafanya bidhaa zinazouzwa ziwe ni zile zilizosindikwa ambapo  Tanzania imedhamiria kufufua mazao ya mkonge, michikichi na mbegumbegu za Mafuta na akawataka watafute wawekezaji makini ambao watakuja kuwekeza kwenye mazao hayo.


Amewataka waangalie ni jinsi gani wanaweza kuinua sekta nyingine kama vile utalii kwa kuitangaza Tanzania huko waendako ili kuvutia watalii wengi zaidi.

 

Akitoa shukrani kwa niaba ya wenzake, Balozi wa Tanzania nchini Uturuki, Luteni Jenerali Yacoub Mohamed alimshukuru Waziri Mkuu kwa nasaha alizowapa na kwamba zimewasaidia kutambua msimamo wa serikali ukoje.

 

Mabalozi hao na nchi zao ni Luteni Jenerali Yacoub Mohamed (Uturuki), Grace Olotu (Sweden), Meja Jenerali Richard Makanzo (Rwanda), Anisa Mbega (India), Innocent Shiyo (Ethiopia), Hoyce Temu (Uswisi) na Togolani Mavura (Jamhuri ya Korea).

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top