} });
 

 

Jeshi la Polisi mkoani Katavi, linamshikilia Seda Mbutula (47) kwa tuhuma za kukutwa na nyara za serikali zidhaniwazo kuwa ni mafuta ya simba, ngozi ya kakakuona, ngozi ya paka pori vipande vinne vya meno ya ngiri na mkia mmoja wa nyumbu.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi Ali Hamad, ambapo amesema tukio hilo limetokea Novemba 23 mwaka huu katika pori la akiba Rungwa lililopo Kata ya Ilunde Wilaya ya Mlele mkoani humo.

Hamad amesema baada ya oparesheni maalumu walifanikiwa kumkamata mtu huyo akiwa amehifadhi nyara hizo kwenye mfuko wa salfeti na kuficha ndani ya nyumba yake.

Sambamba na hilo pia Jeshi la Polisi limemkamata Samweli Kazambi (36) kwa tuhuma za kukutwa na madawa ya kulevya yadhaniwayo kuwa ni bangi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top