} });
 

Na Faustine Gimu Galafoni

Bei ya samaki katika soko la Malya wilayani Kwimba mkoani Mwanza imepanda kutoka 4,000 hadi 6,000 na kuendelea huku chanzo cha kupanda kikitajwa kuwa ni upatikanaji mdogo ziwa Victoria, ubovu wa miundombinu ya barabara kwa ajili ya usafirishaji pamoja  na mahitaji  ya samaki yakiwa ni mengi. 

Wakizungumza na Divine FM baadhi ya wateja  na wafanyabiashara  wa samaki katika soko hilo lililopo pembezoni mwa jiji la mwanza wamesema sababu ya kupanda kwa bei ya samaki ni pamoja na upatikanaji wake kudorora na changamoto za usafirishaji. 

Grace Lugodisha pia ni mmoja wa wafanyabiashara wa samaki wa walikaushwa anasema kupanda kwa bei ya samaki inatokana na kupanda kwa gharama za maisha ikiwemo mafuta yanayotumia kukaangia samaki ambapo hapo awali walikuwa wananunua kwa tsh.32,000 lakini yamepanda hadi 51,000 kwa lita 10  huku katibu wa soko hilo seleman nswizilo akikiri kupanda kwa samaki.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top