} });
 

 

Mwenyekiti wa Kitongoji cha Urua chini, kijiji cha Mfuruashe Wilayani Rombo, Agustine Moshi(35) amemuua mkewe, Anastasia Agustine (31) kwa kumkata kata na kitu chenye ncha kali na kisha mwenyewe kujiua kwa kujinyonga kwa kile kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Mwenyekiti huyo ambaye pia ni mshereheshaji maarufu Wilayani humo (MC), anadaiwa kutenda mauaji hayo usiku wa kuamkia jana Novemba 8, 2021.

Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo jana Novemba 8, Mkuu wa Wilaya ya Rombo, Kanali Hamis Maiga amesema wawili hao walikuwa na mgogoro wa kimapenzi, ambapo wiki moja iliyopita mke wake huyo alimpeleka dawati la jinsia Rombo.

“Huyu jamaa wiki iliyopita mke wake alimpeleka dawati la jinsia hapa wilayani, walisuluhishwa lakini inaonekana halikuisha na ni suala ambalo inaonekana ni wivu wa mapenzi, hivyo akaamua kuchukua jukumu la kumuua mkewe na kisha kujiua kwa kujinyonga,” Maiga.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top