} });
 


Polisi Mkoani Pwani wamesema wanamtafuta Mzee Charles Tulaona Mtweve (67) Mkazi wa Kijiji cha Mafizi Kata ya Gwata Wilaya ya Kisarawe ambaye alitoweka nyumbani kwake November 04,2021 akiwa na wenzake wawili kwenda kuwinda katika pori la Kijiji cha Sungura Morogoro Vijijini na hadi sasa hajulikani alipo.

RPC wa Pwani, Waknyo Nyigesa amesema - ”Mzee Charles akiwa na silaha yake (Shortgun Greener) akiwa amefuatana na Meshack Mkemi (50) na Juma Athmani (40) walikwenda kuwinda na baada ya kuwaua nguruwe pori wawili waliamua kurejea Kijijini Mafizi lakini Charles Mtweve hakufika nyumbani na hadi sasa hajulikani alipo”

“Polisi kwa kushirikiana na Vyombo vingine vya Dola vinafanya ufuatiliaji wa wapi Mzee huyo alipo, kwa Mtu atakayemuona Mzee Mtweve apige simu namba 0712538830 au 0786024709” Waknyo Nyigesa

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top