} });
 

 

Rais Samia Suluhu Hassan amesema serikali yake itaagiza sukari kutoka nchini Uganda ikiwa ni miezi tangu Rais wa Uganda, Yoweri Museveni kuitangazia Tanzania kuwa anaakiba ya kutosha kusaidia kukabiliana na uhaba wa kiungo hicho muhimu.

Akizungumza wakati wa Kongamano la Wafanyabiashara kati ya Tanzania na Uganda, Rais Samia amesema: “Rais (Museveni) aliomba sisi tukanunue sukari kwake, wakasikia statement za waziri wetu kwamba hatutanunua. That was nonsense. Mheshimiwa Rais tutanunua sukari kutoka Uganda.”

Rais Samia ameelekeza mawaziri wa Tanzania kukutana haraka na Mawaziri wa Uganda kuanza kutatua changamoto na vikwazo vinavyo zorotesha biashara kati ya pande mbili.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top