Wafanyabiashara wa gesi wameshauriwa kuwa na mizani ya kupimia ujazo wa gesi ili kuondokana na misuguano baina yao na watumiaji wa mitugi hiyo.
Ushauri huo umetolewa na mwenyekiti wa kamati ya utetezi wa utumiaji wa nishati mkoa wa Geita Dotto Paul wakati akizungumza na watumumiaji wa huduma ya nishati hiyo amesema ili kuondokana na changamoto zinazojitokeza wakati wa ununuzi wa gesi kuna haja ya wauzaji kuwa na mizani ya kupimia mitungi hiyo.
Nao baadhi ya wauzaji wa gesi mjini Meita wamesema mbali na wao kutumia mizani kupimia gesi lakini kuna baadhi yao hawatumii mizani hiyo hali ambayo inazidi kuongeza malalamiko kwa wateja wao.
Hata hivyo wateja wanaonunua mitungi ya gesi wamesema jambo la kutumia mizani kupimia mitungi ya gesi ni jambo zuri na wakaziomba mamlaka kuongeza jitihada za kuwasisitiza wafanyabiashara hao kutumia mizani.
Pia wamesema wamekuwa wakinunua mitungi ya gesi kimazoea hali ambayo inawafanya wakate tamaa kutumia gesi kutokana gharama wanazotumia kununua gesi haziendani na ujazo wa gesi wanaouziwa na wafanyabiashara hao.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment