Shirika la Umeme nchini (TANESCO), limetangaza rasmi kuanza mgao wa umeme wa siku 10 kwa nchi nzima ili kuruhusu matengenezo ya mitambo ya kufua umeme kote nchini. Mgao huo utaanza Februari Mosi hadi 10 mwaka huu.
Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO Maharage Chande, kufuatia taarifa yake ameeleza kuwa ratiba ya mgao huo itatolewa kuruhusu Watanzania na taasisi kupanga ratiba zao na kwamba maboresho katika mtambo wa kufua umeme wa Kinyerezi I na Ubungo III yataongeza uzalishaji kutoka megawati 150 hadi megawati 335.
Facebook Blogger Plugin by TeachMaker
Post a Comment