} });
 

 

Wakiwa safarini kuelekea kwenye harusi ya aliyekuwa mshirika wa Kanisa la Fpct Shalom Temple ndugu Peter Nyakamwe huko Kakonko katika kijiji cha Katanga washirika 7 akiwemo Mzee wa kanisa Abel Luhindu wamenusurika vifo baada ya gari waliyokuwa wamepanda kupinduka mara kadhaa katika kijiji cha Bukiriro.
Akiongea na mwanahabari kwa njia ya simu mmoja kati ya manusura wa ajali hiyo ajulikanaye kwa majina ya Emmanuel Augustino amesema:- "Ajali ilitokea majira ya saa 5 asubuhi siku ya Jumatano tarehe 26 2022 na chanzo kikiwa ni gari kuteleza kwenye kona kisha kuyumba upande wa dereva ndipo dereva alipotaka kuirudisha barabarani na kumshinda, ndipo ilipobinuka mara tatu na Kugonga gema kisha kugeuka Ilikotokea" Emmanuel Augustino mmoja kati ya manusura wa ajali hiyo.
Kwa upande wake kiongozi wa idara ya vijana 'CYM' hapa Fpct Shalom Temple ndugu John Theodory ambae alikuwemo katika gari lililopata ajali amesema:- "Gari zilikuwa mbili moja lilikuwa na watu 8 ambao ni:- Frank Abel, Simon Kamlenga, Audax Adarbath ( dereva) Ezra, Nebati Hussein, Furaha na Raymond Katemi, na gari la pili ambalo ndilo lililopata ajali lilikuwa aina ya Noah na tulikuwemo watu 7 ambao ni Joram Rwassa ambae ndie alikuwa dereva, Mzee Luhindu, Tumaini Philipo, George Jackson,Theodory John , Rouben Charles na Emanuel Augustino. Jumla tulikuwa watu 15 katika msafara huo". John Theodory katibu wa vijana.
Kwa mujibu wa manusura wa ajali hiyo waliojeruhiwa sana ni dereva ndugu Joram Rwassa alieumia eneo la kifua japo kwa sasa anaendelea vizuri, Rouben Charles alieumia eneo la sikio na Mzee wa kanisa Abel Luhindu.
Baada ya ajali kutokea majeruhi hao watatu walikimbizwa kituo cha afya cha Gwanumpu na baadhi yao waliweza kupata huduma hapohapo lakini kwa upande wa dereva ilibidi kukimbizwa mjini Kibondo kwa matibu zaidi kwani ilionekana ameumia eneo la kifua kwani alikuwa hawezi hata kuongea na ilibidi apate msaada wa Oxygen akiwa hapo Hospitali.
Mpaka sasa vijana kadhaa bado wapo Kibondo akiwemo katibu wa CYM ndugu John Theodory wakisubiri kuimarika kwa afya aliyekuwa dereva ndugu Joram Rwassa na wengine wamerejea tayari Kahama.
Tunawaombea majeruhi wote Mungu aimarishe afya zao ili waendelee na majukumu yao ya kila siku.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top