} });
 

 

Kwa mara ya kwanza mwanamuziki kutoka WCB Zuhura Othman maarufu Zuchu amekanusha vikali tetesi za kuhusishwa kutoka kimapenzi na boss wake mwanamuziki Diamond Platnumz.

Tetesi hizo ziliibua mijadala kote mitandaoni kwa kipindi cha miezi kadhaa bila ya yeyote kati ya wahusika kutoa kauli juu ya undani wa suala hilo kasi cha kuacha mashabiki wa wasanii hao wakiendelea kubashiri hadi kufikia hatua ya kuenea kwa uvumi kuwa wawili hao wako mbioni kufunga ndoa.

“Ni boss wangu. Diamond ni boss wangu kila siku, hajawahi kubadilika. Nina date na mtu, nina boy friend ndio, lakini ni mtu wa kawaida tu.” Alisema.

Zuchu ameyasema hayo Kupitia mahojiano maalum aliyoyafanya na kipindi cha mashasham, ambapo ameweka wazi suala hilo baada ya kuulizwa kuhusu undani wa fununu hizo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top