Na Daniel Manyanga - Simiyu
Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, David Kafulila amewataka wananchi Wilayani Maswa kuendelea kuchangia fedha kwa ajili ya kuwalipa walimu wanaojitolea kwenye shule za msingi na sekondari.
Ombi hilo amelitoa kufuatia hoja iliyoibuliwa na mwananchi juu ya upungufu wa walimu 852 kwa shule ya msingi kati ya 1200 waliopo kwa sasa, huku Sekondari kukiwa na upungufu wa walimu 186 kati ya 556.
Aidha ameitaka Wakala wa Barabara za Mjini na Vijijini (TARURA) Wilayani hapa kuhakikisha wanakamirisha kwa wakati ujenzi na ukarabati wa Barabara kufuatia malalamiko ya wananchi kuilalamikia TARURA kwa ubovu wa miundo mbinu.
Kwa upande wa waraghbishi Wilayani hapo wamebainisha adha wanazokabiliana nazo kutokana na ukosefu wa miundombinu vijijini mwao.
Akitolea ufafanuzi wa changamoto za barabara Meneja TARURA Wilayani hapa amewaomba wananchi kuendelea kuzifungua Barabara ili ziweze kuingizwa kwenye mtandao wa Barabara za Tarura.
Post a Comment