Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini yaliyofanyika kwenye viwanja vya Chinangali, jijini Dodoma leo. |
Rais Samia
Suluhu Hassan ameitaka mahakama kuzingatia sheria ili kutenda haki kwa watu
wote bila kujali hali ya mtu kijamii na kiuchumi.
Rais
Samia ameyasema hayo leo Jumatano Februari 2, 2022 wakati wa kilele cha
maadhimisho siku ya sheria nchini yaliyofanyika katika viwanja vya Chinangali
jijini Dodoma.
Amesema
anatambua mageuzi yanayoendelea katika mahakama yameongeza uwazi na uwajibikaji
kwa watendaji wa mhimili huo lakini bado yapo malalamiko kwa wananchi ya
kucheleweshewa haki na wakati mwingine kunyimwa kabisa.
Mkuu huyo
wa nchi amesema malalamiko hayo yako hususani kwenye mirathi na hasa kutoka kwa
wanawake wajane na migogoro ya ardhi.
Aidha,
Rais Samia ameitaka mahakama kutoa haki bila kufungwa na masharti ya kiufundi
ambayo wananchi wengi hawafahamu na wanategemea mawakili ndio wawaongoze.
Pia
ameitaka mahakama kutekeleza majukumu yake kwa kuangalia utu wa mtu kwa yule
anayetoa hukumu na anayepewa.
“Utu
wako unakutumaje uchukue fedha uminye haki ya mtu? Au umpe aliyetumia umahiri
na vifungu kumyima haki mwenye haki,”amehoji Rais Samia.
Post a Comment