} });
 

 

Na Faustine Matalange - Katavi

Shirika la kukuza viwanda vidogovidogo SIDO katika mkoa wa Katavi limeanza Mpango wa kuwakopesha wajasiriamali ili kujikwamua kiuchumi Kwa kuwakopesha shilingi Milion 42. 

Hayo yamebainishwa na kaimu meneja wa SIDO mkoa wa Katavi Salome Mwasomola wakati wa hafla ya kukabidhi mikopo hiyo amesema SIDO imeanza kutekeleza mpango huo kwa vitendo kwa kutoa mikopo hiyo ambapo wajasiliamali wapatao 48 wamenufaika na mpango huo. 

Awali akitoa neno kwa wajasiliamali hao kaimu mkuu wa wilaya ya Mpanda Onesmo Buswelu amesema, serikali imekuwa ikiandaa mazingira wezeshi Kwa wajasiriamali kwa kuja na mipango mbalimbali ya kuwajali Ili wajikwamue kiuchumi na kuwaomba kutumia mikopo hiyo kwa malengo yaliyo kusudiwa. 

Kwa upande wao wajasiliamali hao wamesema mikopo hiyo itawasadia pakubwa katika kuimalisha shughuli zao kwa kuwa haina riba na kuishukulu serikali kwa kuja na mpango kupitia shirika la SIDO. 

Licha ya serikali kuendelea kutoa mikopo kwa makundi ya wanawake walemavu na vijana, serikali bado imeanza mpango wa kutoa mikopo kwa wajasiriamali kupitia shirika la SIDO mkoa wa Katavi.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top