} });
 


Uongozi wa Simba SC umetoa taarifa ya kuwashukuru Mashabiki waliojitokeza Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa ajili ya mchezo wa Mzunguuko wa Kwanza wa hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika dhidi ya ASEC Mimosas ya Ivory Coast.

Simba SC imetoa taarifa ya shukurani kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii ambapo imekiri kuwa mashabiki waliojitokeza Uwanja wa Mkapa ndio walikua kichocheo cha ushindi wa 3-1, uliopatikana jana Jumapili (Februari 13).

Pia taarifa hiyo imewasihi Mashabiki wa Simba SC kutowabugudhi mashabiki wa klabu nyingine ambao hujitokeza Uwanjani kushuhudia michezo ya kimataifa ya klabu hiyo.


Wakati Simba SC ikiaanza kwa ushindi wa 3-1, RS Berkane ya Morocco nayo imeanza kwa kuibamiza US Gendamarie ya Niger kwa mabao 5-3, hivyo kulifanya Kundi D kuwa na timu mbili zenye alama 3.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top