} });
 

 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mohamed Mchengerwa jana Februari 14, 2022 ametoa maelekezo kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) yanayolenga kuboresha mchezo wa mpira wa miguu nchini.

Maelekezo hayo ameyatoa katika mkutano wa Waandishi wa Habari aliofanya katika Ukumbi wa Uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam jana Februari 14 baada ya kufanya kikao na Viongozi wa TFF, BMT na watendaji wa Wizara.

Amefafanua kuwa Serikali ipo katika mikakati kabambe ya kuboresha miundombinu ya michezo katika shule 56 nchini ikiwa ni pamoja na kufunga mashine za kisasa za kufuatilia michezo (VAR) kwenye viwanja vitano kwa kuanzia pamoja na kujenga vituo vikubwa vya michezo.

Akitoa maelekezo ya Serikali, Mchengerwa amesema BMT likutane na TFF mara moja kujadili namna ya kudhibiti vitendo vya ukiukwaji wa Sheria na taratibu za mchezo huo pendwa nchini ambapo pia amesisitiza kuwa Kamati inayohusika na Waamuzi ijitafakari kwa kuwa hadi sasa kwenye msimu huu wa ligi tayari imeshawaondoa waamuzi 13 kwa makosa ya upendeleo na rushwa.

Pia amesema TFF likutane na waamuzi wote ili kupata uvumbuzi wa changamoto na sintofahamu zinazoendelea kujitokeza katika mchezo huo kinyume na sheria ambapo TAKUKURU washirikishwe wawepo ili waweze kutoa elimu ya rushwa kwenye mchezo wa mpira wa miguu.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top