} });
 

 

Na Nyamiti Alphonce Nyamiti

Wananchi wa kata ya Mwalugulu katika halimashauri ya Msalala wamepongeza jitihada za Mbunge wa Jimbo hilo Mh Iddy Kassim Iddy kushirikiana na Serikali katika Utekelezwaji wa miradi ya Maendeleo katika sekta ya Maji,Afya,Barabara na Elimu.

Wameyabainisha hayo kwenye sherehe ya miaka 45 ya kuzaliwa kwa Chama Cha Mapinduzi zilizoazimishwa ferb 26 mwaka huu katika Kijiji cha kirimbu.

"Tunapendezwa na jitihada za mh mbunge wetu Iddy Kassim Iddy kwa namna anavyo tusaidia sisi wananchi wake Tunamuombea kwa Mungu aendelee hivyo hivyo" Walisema wananchi

Akitoa taarifa ya utekelezwaji wa Shughuli za Maendeleo Diwani wa kata hiyo Mh Frola Sagasaga Amesema kwa kitu cha Afya kwenye kata hiyo kutasaidia kutatua kero ya Wananchi kufuata matibabu kwa umbali mrefu na kupata matibabu kwa haraka Hususani kwa Wanawake na watoto.

"Mh Mbunge tungekuwa na kilimo cha mda mrefu hapa katika upatikanaji wa huduma za afya kwani wananchi Hawa hulazimika kwenda hospitali ya wilaya kupata matibabu" Alisema Diwani sagasaga

Kwaupande wake Mh Iddy Amesema Kwakipindi chake chote cha Uongozi wake kwa miaka mitano atahakikisha anawapigania Wana msalala kupata Maendeleo hasa katika sekta ya afya ambayo Bado ni changamoto kwa msalala

"Naomba niendelee kuwaahidi wananchi tangu mlipo Nipa ubunge mwaka 2020 niliahidi na ninasema nitaendelea kuwatumikia kwa kuwapigania Maendeleo" Alisema Iddy Kassim Iddy.

Ikumbukwe kuwa Iddy Kassim Iddy amekuwa mbunge wa Jimbo la msalala tangu mwaka 2020 na kufanikisha ujenzi wa vituo vya afya na dhahanati kwenye kata ya Isaka,Mwalugulu imeingiziwa tsh 250 kuanza ujenzi wa kituo cha Afya,Segese hatua za ujenzi wa kituo cha afya zimeanza,zahanati za mwankima,kabondo,na matinje, zimeingiziwa kiasi cha Tsh mil 150 kwaajiri ya vifaa Tiba.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 1. I think this is one of the most significant information for me.
  And i’m glad reading your article.
  But should remark on some general things, the web site style is perfect,
  the articles is really great
  wordpress
  blogspot
  youtube
  ប្រដាល់ថៃ

  ReplyDelete

 
Top