} });
 

 

Filamu ya Royal Tour ambayo ilirekodiwa Tanzania miezi michache iliyopita kwa lengo la kutangaza vivutio vya utalii hatimaye imezinduliwa Jijini New York, Marekani jana April 18 2022 na kutazamwa na Watu mbalimbali wakiongozwa na Rais wa Tanzania Samia Suluhu Hassan.

Baada ya kuitazama filamu hiyo Rais Samia aliketi jukwaani na kuulizwa maswali machache na Watu mbalimbali pamoja na Mtangazaji na Muandaaji wa filamu hiyo Peter Greenberg ambapo hakusita kuinadi Tanzania kuwa sehemu nzuri ya kutembelea na yeyote atayekwenda hatojutia uamuzi wake

Aidha rais alibainisha kuwa filamu hiyo ilimfanya aendeshe gari kwa mara ya kwanza baada ya miaka 15.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top