} });
 

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla amesema kwa sasa Mkoa upo shwari kufuatia oparesheni kabambe ya kuwakamata Panya Road waliokuwa wakifanya matukio ya uhalifu maeneo mbalimbali ya Dar es Salaam.

RC Makalla amesema mpaka sasa oparesheni imefanikiwa kuwafikisha Mahakamani Watuhumiwa 35 na wengine 17 wanaendelea kufanyiwa uchunguzi.

Kutokana na Hilo RC Makalla amewatoa hofu Wananchi na kulipongeza Jeshi la Polisi kwa kazi kubwa na nzuri waliyoifanya kuvunja uti wa mgongo wa mtandao mzima wa Panya Road

Ili kuhakikisha matukio Kama hayo hayajirudii, RC Makalla amesema wameweka mpango mkakati endelevu kwa kudhibiti uhalifu wa aina yoyote usitokee Dar es Salaam.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top