} });
 

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini

Mbunge wa Viti Maalum, Fatuma Toufiq ameibua sakata la kikundi cha uhalifu maarufu Panya Kalowa ambacho amesema kinawasumbua wananchi wa Kata ya Dodoma Makulu jijini Dodoma.

 

Toufiq ametoa kauli hiyo wakati akiuliza swali la nyongeza bungeni leo Jumatatu Juni 13, 2022 ambapo amesema kuwa kumeibuka kikundi hicho kinachoumiza wananchi.

 

“Mheshimiwa Naibu Spika kumeibuka kikundi kinachoitwa panya kalowa ambacho kinaumiza watu, nataka kujua Serikali inachukua hatua gani kudhibiti kikundi hicho ambacho ni hatari kwa wananchi,” amehoji Toufiq.

 

Swali la mbunge huyo limekuja huku kukiwa na matukio mengi ya ukabaji na mauaji yanayoripotiwa katika maeneo kadhaa ya Jiji la Dodoma huku Kata za Chang’ombe na Dodoma zikiongoza kuwa na matukio mengi.

 

Akijibu swali hilo, Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Jumanne Sagini amesema Serikali inazo taarifa kuhusu kikundi hicho na makundi mengine na tayari wameanza kuwashughulikia.

 

Sagini amesema tayari kuna baadhi ya vijana ambao wamekamatwa na Jeshi la Polisi Mkoa wa Dodoma wakitokea maeneo hayo lakini kazi zaidi inafanyika kuwabaini wahusika wote.

 

Hata hivyo ametoa wito kwa wananchi kuendelea kushirikiana na polisi katika kuwapatia taarifa sahihi ili waweze kuwabaini vijana wote kwenye makundi hayo.

 

Hivi karibuni kuliibuka kundi la vijana maarufu Panya Road liliibuka na kuvamia baadhi ya mitaa ya jijini Dar es Salaam huku vijana hao wakipora na kujeruhi watu.

 

Hata hivyo Mei 18 mwaka huu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla alisema vijana 35 wanaojihusisha na vitendo vya kihalifu maarufu ‘Panya Road’ wamefikishwa mahakamani huku uchunguzi wa wengine 17 ukiwa unaendelea.


soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top