} });
 

Farid Mussa amesaini Mkataba wa miaka miwili Jangwani

MCHEZAJI wa Yanga Farid Mussa ameongeza mkataba wa miaka miwili ambao utamfanya aendelee kuwepo katika viunga vya Jangwani hadi mwaka 2024

 

Farid amekuwa na msimu mzuri kutokana na kuwa na uwezo wa kucheza katika nafasi mbalimbali ikiwemo mlinzi wa kushoto, winga wa kushoto na kulia, kiungo wa kati na kiungo mshambuliaji.

 

Farid Mussa ambaye amewahi kucheza soka nje ya nchi katika klabu ya Tenerife ya nchini Hispania alianza maisha yake ya soka katika klabu ya Azam ambapo baada ya kufanya vizuri ndipo akapata dili hilo la kwenda nchini Hispania.


Kulikuwa na tetesi hivi karibuni zikimhusisha kujiunga na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara Klabu ya Simba ambapo kwa mkataba huo mpya ni wazi kwamba Farid Mussa ataendelea kuwa mchezaji muhimu kwenye kikosi cha mabingwa hao wa muda wote wa Ligi Kuu Bara.

 

Kwa upande mwingine Farid Mussa amebainisha kuwa kuanzia sasa atakuwa chini ya Meneja wake mpya Oscar Oscar ambaye atasimamia masuala yake ya kisoka.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top