} });
 

 

Makada wa zamani 19 wa Chadema na wabunge wa viti maalumu, waliovuliwa uanachama wa chama hicho, Halima Mdee na wenzake 18, leo wanatarajiwa kuchuana vikali kwa hoja za kisheria na chama hicho mahakamani wakati maombi yao yatakaposikilizwa.

 

Mdee na wenzake wamekwenda mahakama kupinga uamuzi wa chama hicho kuwavua uanachama na wamefungua maombi Mahakama Kuu, dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, wakiomba kibali cha kufungua shauri la mapitio ya kuhusu uamuzi huo.

 

Sambamba na maombi hayo, pia wamefungua maombi ya zuio la muda dhidi ya ubunge wao kusubiri usikilizwaji na uamuzi wa maombi yao ya kibali cha kufungua kesi.

 

Maombi hayo yote yamepangwa kusikilizwa leo na Jaji John Mgetta na mawakili wa pande zote watachua kwa hoja za kisheria.

 

Katika usikilizwaji wa maombi hayo, jopo la mawakili wa kina Mdee linaloongozwa na wakili Aliko Mwamanenge litakuwa na kibarua cha kuishawishi mahakama kuridhia amri ya zuio la muda dhidi ubunge wa wateja wao na pia kuridhia kutoa kibali cha kufungua shauri rasmi la kupinga kuvuliwa uanachama wao.

 

Lakini jopo la mawakili wa Chadema linaloongozwa na Peter Kibatala, litakuwa na kibarua kuishawishi mahakama kuwa haistahili kutoa amri hiyo ya zuio la muda dhidi ya hatua zozote zitakazoathiri ubunge wao wala kibali cha kufungua shauri la kupinga kuvuliwa kwao uanachama.

 

Mdee na wenzake walichukua hatua hiyo baada ya uamuzi wa Baraza Kuu la Chadema kutupilia mbali rufaa zao za kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho, kuwavua uanachamaNovemba 27,2020.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top