} });
 

Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam linamtafuta mtuhumiwa Zheng Lingyao (42), raia wa China na mkazi wa jiji hilo kwa tuhuma za kumuua Fu Nannan (26) raia wa China mfanyabiashara na mkazi wa Kalenga Ilala, uchunguzi umebaini kulikuwa na tatizo la masuala ya mapenzi.

Taarifa hiyo imetolewa Juni 12, 2022, na Kamanda wa Polisi wa Kanda hiyo, ACP Jumanne Muliro, ambapo amesema tukio hilo imetokea Juni 11, 2022, mtaa wa Kalenga Ilala, kwenye ghorofa ya tatu ya wapangaji majira ya saa 5:40 usiku.

"Mtuhumiwa anayetafutwa alifika eneo hilo na kumjeruhi kwa risasi tumboni Nie Mnqino (32) raia wa China na baadaye alimfyatulia risasi Fu Nannan alipoteza maisha na Nie anaendelea na matibabu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, uchunguzi wa awali wa tukio hili umebaini kuwepo kwa tatizo la kutoelewana lililotokana na masuala ya kimapenzi,"amesema Kamanda Muliro

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top