Waziri wa Fedha na
Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema katika mwaka 2021 mfumuko wa bei uliongezeka
kwa wastani wa asillimia 3.7 ikilinganishwa na wastani wa asilimia 3.3 mwaka
2020.
Dk Mwigulu
amesema hayo leo Jumanne Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha hali ya uchumi wa
Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2022/23.
Amesema mfumuko
wa bei umeendelea kuwa ndani ya lengo la wigo wa asilimia 3 hadi 5.
“Mfumuko wa
bei ulifikia wastani wa asilimia 3.8 Aprili 2022 ikilinganishwa na asilimia 3.3
Aprili 2021.
“Kuongezeka kwa mfumuko wa bei kulichangiwa na sababu zilizo nje ya udhibiti wa Serikali zikiwemo kuvurugika kwa mnyororo wa uzalishaji na usambazaji wa bidhaa na huduma katika soko la dunia kutokana na athari za vita baina ya Urusi na Ukraine” Dk Mwigulu
Post a Comment