![]() |
Juma Raibu akizungumza baada ya kuchukua
fomu ya kuwania nafasi ya Meya Manispaa ya Moshi, Raibu aliondolewa kwenye
nafasi hiyo baada ya kupigiwa kura ya siri na madiwani. Picha na Florah Temba |
Meya wa zamani wa
Manispaa ya Moshi mkoani Kilimanjaro, Juma Raibu aliyevuliwa wadhifa huo baada
ya kupigiwa kura za siri na madiwani za kukataliwa amejitokeza tena kuchukua
fomu ya kuomba kuteuliwa na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuwania nafasi hiyo.
Juma Raibu
aling'olewa katika wadhifa huo Aprili 11 mwaka huu, baada ya madiwani kupiga
kura za siri na kati ya kura 28 zilizopigwa, 18 zilikataa asiendelee na wadhifa
huo huku 10 zikimtetea abaki katika nafasi hiyo aliyodumu nayo tangu
ulipokamilika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020.
Tuhuma zilizomng'oa
Raibu ni madai ya kuhudhuria sherehe ya kijana mmoja anayedaiwa kushiriki
mapenzi ya jinsia moja, kutumia vibaya ofisi yake, kujihusisha na vitendo vya
rushwa, kuruhusu ujenzi holela na kutumia fedha nje ya utaratibu.
Akizungumza
mara baada ya kuchukua fomu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Moshi
mjini, Raibu amesema ameamua
kurudi kuwania nafasi hiyo kwa kuwa toka ameondolewa kwenye nafasi hiyo, baada
ya kuona Moshi imepoa na kuwepo kwa vurugu nyingi.
"Moshi
imelala, siyo Moshi niliyokuwa nikiiongoza, nimeona ni wakati wa kurudi
kuchukua nafasi hii, ninaamini tutashirikiana na madiwani katika kuiendeleza Moshi.
Amesema zaidi ya wananchi 500 wamefika nyumbani kwake
kumuomba na kumchangia ili aweze kurudi kugombea nafasi hiyo.
"Niliwakatalia
wananchi na kutaka kupeleka fedha hizi kutoa sadala, lakini walikataa wakataka
nije nichukue fomu na niwaambie nipitishwe au nisipitishwe, nitaendekea kuwa
mwanachama wa CCM"
Katibu wa CCM
Moshi Mjini, Ibrahim Mjanakheri amesema tangu kuanza mchakato wa kuchukua fomu
Juni 12, tayari wamechukua madiwani nane.
Amewataja
Madiwani hao kuwa ni Apaikunda Nabuli, Francis Shio, Zubery Kidumo, Charles
Lyimo, Stuart Nkinda, charles Mmbando, Nasibu Mariki na Juma Raibu.
Post a Comment