Waziri wa
Fedha na Mipango, Dk Mwigulu Nchemba amesema inakadiriwa kuwa jumla ya Sh15.8
bilioni sawa na asilimia 36.2 ya Bajeti yote ya Serikali zitatumika kugharamia
miradi ya maendeleo ikijumuisha miradi ya huduma za jamii kwa mwaka 2022/23.
Dk
Nchemba amesema hayo leo Jumanne Juni 14, 2022 wakati akiwasilisha hali ya
uchumi wa Taifa na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa mwaka wa fedha 2022/23.
“Kati
ya kiasi hicho, Sh12.8 bilioni sawa na asilimia 82.0 ya bajeti ya maendeleo ni
fedha za ndani na Sh2.1 bilioni sawa na asilimia 18.0 ya bajeti ya maendeleo ni
fedha za nje.” Amesema Dk Mwigulu
Amesema katika kuongeza ushiriki wa sekta binafsi kama injini muhimu ya utekelezaji wa miradi, Serikali itahakikisha miradi yote inayovutia uwekezaji wa sekta binafsi inatekelezwa kwa utaratibu wa Ubia kati ya Sekta ya Umma na Sekta Binafsi (PPP) na Joint Venture kwa kutumia utaratibu wa Kampuni Maalumu (Special Purpose Vehicle).
Post a Comment