} });
 

Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev akiwa na Rais wa sasa wa Urusi Vladimir Putin

NCHI ya Urusi imeonya kuwa kuna uwezekano wa Bara la Ulaya kupotea kwa bomu la nyuklia kutokana na kitendo cha mataifa ya magharibi kutoa misaada ya zana za kivita ikiwemo mabomu na makombora ya masafa marefu nchini Ukraine.

 

Viacheslav Volodin ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Usalama nchini Urusi ameyasema hayo baada ya kauli ya Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje wa Poland Radoslaw Sikorski aliyesema kuwa nchi za magharibi zitaendelea kupeleka zana zaidi za kivita nchini Ukraine ikiwemo mabomu ya nyuklia ili nchi hiyo iweze kujilinda na uvamizi wa Urusi.


Sikorski amemshukia Rais wa Urusi Vladimir Putin kwa kudai kuwa amekiuka mkataba wa makubaliano ya Amani wa Budapest uliosainiwa mwaka 1994 na hivyo kutoa mwanya kwa nchi za magharibi kuisaidia Ukraine zana za kivita kiwemo mabomu ya nyuklia ili iweze kutetea uhuru wake.

 

Waziri huyo wa zamani aliiambia chaneli ya Ukraine ya Espreso TV kuwa nchi za magharibi hazina namna nyingine zaidi ya kutoa msaada wa zana za nyuklia.

 

Kwa mujibu wa taarifa na rekodi za usalama ni kwamba Ukraine ilikubali kuachana na zana za nyuklia mara tu baada ya kuanguka kwa utawala wa kisovieti na hivyo kusaini mkataba maalum wa kupinga matumizi ya zana za nyulia ujulikanao kama Nonproliferation.


Kwa upande mwingine Volodin kupitia mtandao wa Telegram amesema:

“Kwa maamuzi hayo Ulaya itapata matatizo makubwa sana kuliko haya wanayoyapata kwa sasa (Wakimbizi, Ongezeko la bei na Uhaba wa nishati), kwa sababu anachokifanya Sikorski ni kuhamasisha mgogoro wa vita za nyuklia baina ya mataifa ya Ulaya, hajali kuhusu usalama wa Ukraine au hatima ya usalama wa Poland.

 

Naye Rais wa zamani wa Urusi Dmitry Medvedev ameonya kuwa Urusi itatumia silaha na mabomu ya nyuklia kama Ukraine itatumia makombora kutoka Marekani na nchi za Ulaya Magharibi.

 

Medvedev aliyekuwa rais kuanzia mwaka 2008-2012 alinukuliwa akisema:

“Nimekuwa nikikosolewa kuhusu machapisho yangu kwenye mtandao wa Telegram kwamba ni makali sana. Jibu ni kwamba nawachukia kwa sababu hawapendi usalama wa Urusi wanataka Urusi iangamie lakini kwa kuwa bado nipo hai ntapambana hadi mwisho kuona kitu hicho hakitokei zaidi wataangamia wao.”

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top