} });
 


SERIKALI ya India imefikia maamuzi ya kuvunja nyumba za wanaharakati na waandamanaji wa Kiislam katika Jimbo la Utter Pradesh walioandamana kupinga kauli ya kibaguzi dhidi ya dini ya kiislam iliyotolewa na moja ya wanasiasa wenye nguvu nchini India akiwemo Nupur Sharma.

 

Tayari Polisi wamefanikiwa kuwatia nguvuni watu 300 kutokana na maandamano hayo.

 

Kwa mujibu wa Shirika la Utangazaji la Uingereza BBC limesema kauli hiyo imefichwa kutokana na kama ikichapishwa inaweza kuleta tafsiri hasi na machafuko zaidi miongoni mwa wanajamii.

 

Baada ya kauli hiyo ya Sharma ilisababisha maandamano ndani ya maeneo ya jimbo la Utter Pradesh ndipo Waziri Mkuu wa Jimbo hilo alipotoa amri ya kuvunjwa kwa nyumba ya baadhi ya viongozi wakuu wa dini ya kiislam katika Jimbo hilo.

 

Moja ya nyumba iliyobomolewa ni ya mwanasiasa Javed Ahmed, gazeti la Hindustan Times linaloandika habari zake kwa lugha ya Kiingereza limeripoti kuwa mtoto wa Javed anayefahamika kwa jina la Afreen Fatima ni mwanaharakati mkubwa anayepigania haki ya dini ya kiislam nchini humo nay eye ndiye chanzo cha nyumba yao kubomolewa.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top