} });
 

Billionea Elon Musk (Anayetaka kuachana na mpango wa kuinunua twitter)

Tajiri nambari moja duniani Elon Musk ametangaza rasmi kuachana na mpango wake wa kununua mtandao wa Twitter kwa gharama ya dola za kimarekani billioni 44, sababu kubwa iliyopelekea uamuzi huo wa Elon Musk ni kutokana na kukosa ushirkiano kutoka kwa wamiliki wa twitter kwa kumruhusu bilionea huyo kufanya uchunguzi juu ya akaunti feki zilizosajiliwa kwenye mtandao wa Twitter.

 

Taarifa hii iliwasilishwa kwenye bodi ya Twitter kwa njia ya barua kutoka kwa Elon Musk kupitia Wakili wake.

 

Kwa upande wao bodi ya mtandao wa Twitter wao wamesema kwamba wako kwenye hatua ya kuchukua hatua za kisheria ili kuhakikisha kwamba makubaliano waliyowekeana na billionea huyo yanatizwa ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kwamba Elon Musk anafanya malipo kwa ajili ya kuununua mtandao huo kama walivyokuwa wamekubaliana hapo awali.

 

Hatua hizo za kisheria zinatarajiwa kuchukua nafasi yake kwenye mahakama inayojulikana kama Dalaware court of Chancery huko nchini Marekani.

 

Hii inatokea ikiwa ni miezi miwili tangu billionea Elon Musk alipotangaza nia yake ya dhati ya kuununua Mtandao   huo wa Twitter.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top