} });
 

 

MSHAMBULIAJI wa klabu ya Bayern Munich na Timu ya Taifa ya Poland Robert Lewandowski amesalimu amri na kukubali yaishe baada ya kuamua kurudi katika viunga vya Bavarians na kujiandaa kwa ajili ya maandalizi ya msimu mpya wa 2022/2023.

 

Taarifa za awali zilidai kuwa Lewandowski aligomea kurudi klabuni hapo akishinikiza Bayern kukubali ofa ya FC Barcelona ili kumruhusu mshambuliaji huyo hatari mwenye umri wa miaka 34 kujiunga na miamba hiyo ya soka duniani ili aweze kutimiza ndoto zake za kucheza Nou Camp.

 

Bayern Munich wameendelea kushikilia msimamo wao kwa kukataa ofa zaidi ya tatu kutoka kwa FC Barcelona wakisistiza kutaka kiasi cha Euro Milioni 40 kama ada ya kumruhusu Lewandowski kuondoka klabuni hapo.

 

Mkataba wa Lewandoski na Bayern Munich unatarajiwa kumalizika mwezi Juni mwaka 2023. Ambapo kuanzia hapo mchezaji huyo atakuwa huru kujiunga na klabu yoyote aitakayo.


Lewandowski amegoma kusikiliza ofa kutoka vilabu vingine ikiwemo klabu ya Chelsea ya nchini Uingereza huku akisisitiza malengo yake akiondoka Bayern Munich ni kuichezea FC Barcelona tu.

 

Taarifa kutoka nchini Ujerumani zimebainisha kuwa Lewandowski atapewa programu maalumu na Kocha Nagelsmann, huku ikisistizwa kuwa kama ndoto yake ya kujiunga na Barcelona haitakamilika basi Lewandowski atamalizia mkataba wake na kufanya kazi kwa kuzingatia weledi hadi mwisho wa mkataba wake

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top