} });
 

Balozi wa Marekani Nchini Tanzania Donald wright akiwa kwenye mazungumzo na Rais Samia Suluhu

SERIKALI ya Marekani imesema kwamba ipo tayari kutoa ujuzi na ushauri kwa Tanzania kahusiana na masuala ya kiusalama kwa lengo kuimarisha ulinzi kwenye mpaka wake na nchi ya Msumbiji.

 

Balozi wa Marekani nchini Tanzania Donald Wright alifafanua juu ya namna ambavyo Marekani inaguswa na tishio la usalama lililopo katika baadhi ya mipaka ya Tanzania ikiwemo eneo la mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.


Aidha ameelezea athari ya mabadiliko ya tabia nchi lakini pia hatua iliyopigwa na serikali ya Tanzania katika kukuza demokrasia.


Balozi Wright alisema, “Kimsingi Marekani inaguswa na masuala ya kiusalama ya dunia nzima, na hata ukiangalia masuala ya kiusalama katika mipaka ya kusini mwa Tanzania. Kama Balozi natambua na kuweka suala hilo kuwa kipaumbele cha ubalozi wangu”


Pia alisema “tunafikiri kwamba masuala haya yasipoangaliwa kwa umakini yanaweza kuleta madhara, hivyo tumekuwa tukijielekeza katika masuala haya, na tunafurahi kuona Rais Samia Suluhu ameushirikisha umoja wa nchi za kusini mwa SADC ili ziweze kutoa suluhisho na sisi tupo tayari kutoa ushirikiano wetu wa kimawazo pale utakapo hitajika.”


Katika hatua nyingine Balozi huyo amepongeza jitihada zinazofanywa na serikali ya Tanzania ya sasa kutokana na mazungumzo ambayo yamekuwa yakiendelea kati ya serikali, chama tawala na vyama vya upinzani.


Balozi huyo alisema kwamba Rais Samia ameonyesha jitihada kubwa katika suala zima la maridhiano ya kisiasa amekuwa na mikutano kadha kukutama na viongozi wa upinzani ili kupata mariadhiano ya kisiasa na kupata maoni yao hivyo sisi Marekani tunasimama na serikali na kwamba tunaunga mkono kufikiwa kwa maridhiano hayo. 

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top