![]() |
Nyumba ya Waziri Mkuu wa Sri-Lanka ikiteketea kwa moto |
Nyumba ya Waziri mkuu wa Sri Lanka Ranil Wickremesinghe imechomwa moto katika ghasia za waandamanaji ambao wamekusanyika kwa pamoja kupinga hali ngumu ya maisha inayowakabili nchini humo.
Awali maelfu ya waandamanaji wamevamia kamazi ya Rais Gotabaya Rajapaksa katika mji mkuu wa Sri Lanka.
Taarifa za awali zilizotolewa zilisema kuwa rais alikuwa ameondolewa tayari na kupelekwa katika eneo salama wakati waandamanaji walipoingia kwenye makazi yake.
Nchi hiyo inakabiliwa na mfumuko mkubwa wa bei za bidhaa na inahangaika kuagiza chakula, mafuta na madawa kutoka mataifa mengine ya jirani.
Maelefu ya waandamanaji wanaoipinga serikali walisafiri hadi katika mji mkuu, huku maafisa wakiliambia shirika la habari la AFP kwamba wengine hata ‘’waliziamrisha’’ treni kufika pale.
Takriban watu 33, wakiwemo wanajeshi wa usalama, wamejeruhiwa na wamekuwa wakipata matibabu katika hospitali ya taifa ya Sri Lanka mjini Colombo, msemaji wa hospitali hiyo amewaeleza waandishi wa habari.
Maafisa wa polisi na vikosi vingine vya usalama nchini humo walijaribu kuzuia maandamano hayo yasifanyike kwa kuweka katazo la watu kutoka nje usiku wa ijumaa, Lakini katazo hilo halikufua dafu kwani waandamanaji hao hawakukata tamaa jambo ambalo lilipelekea amri hiyo ikaondolewa baada ya makundi ya kiraia na vyama vya upinzani kuipinga vikali na kuingia barabarani kwa maandamano hayo makubwa.
Waziri mkuu Ranil Wickremesinghe ameitisha mkutano wa dharura wa viongozi wa vyama vya kisiasa vya Sri Lanka kujadili mzozo huo lakini pia amemuomba Spika kikao cha bunge.
Post a Comment