} });
 

 

KIUNGO raia wa Ufaransa Paul Pogba amekamilisha usajili wake wa kujiunga kwa mara nyingine na miamba ya soka nchini Italia Juventus kwa kusaini mkataba wa miaka mine akitokea klabu ya Manchester United kama mchezaji huru.

 

Kabla ya kurudi tena Juventus kwa mara ya pili Pogba alianzia maisha yake ya soka akiwa na klabu ya Manchester United ambapo aliamua kujiunga na Juventus kabla ya kutimka na kujiunga tena na Manchester United kwa ada ya uhamisho wa dunia ya Paundi milioni 89 mnamo mwaka 2016.

 

Pogba ameitumikia Manchester United kwa kipindi cha miaka 6 ambapo amekuwa na kipindi cha kushuka na kupanda kwa kiwango huku akifanikiwa kufanya kazi na makocha mbalimbali akiwemo Mreno Jose Mourinho.

 

Akiwa na Juventus Pogba alifanikiwa kufunga jumla ya mabao 34 na kutoa pasi 40 za mabao katika jumla ya michezo 178 katika msimu wake wa kwanza akiwa na miamba hiyo ya soka nchini humo.


Pogba (29) amekabidhiwa jezi namba 10 na kupewa mshahara wa takribani Euro milioni 8 kwa mwaka pamoja na bonasi mbalimbali huku pia akipewa pesa ndefu kwa ajili ya usajili.

 

Juventus inamuona Pogba kama moja ya wachezaji muhimu katika harakati zake za kuboresha kikosi cha timu hiyo ili iweze kurudisha utawala wake nchini humo hasa baada ya kukosa kombe la Scudetto kwa misimu miwili mfululizo.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top