} });
 

 

MAHAKAMA mjini Barcelona imeidhinisha uchunguzi wa mwili wa aliyekuwa Rais wa Angola, Jose Eduardo dos Santos ufanyike.

 

Alifariki katika jiji la Barcelona, Hispania siku ya Ijumaa, alikokuwa ameenda kwa matibabu. Uchunguzi wa maiti uliombwa na binti yake na marehemu dos Santos, aitwaye Tchize dos Santos.

 

Amezungumzia njama ya kumuua babake ili kumzuia kuunga mkono upinzani katika uchaguzi ujao wa Angola.


Mawakili wa familia ya Dos Santos wameshutumu hatua za serikali ya Angola kurudisha mwili wa marehemu Angola kwa mazishi ya kitaifa, dhidi ya matakwa ya Rais huyo wa zamani kuzikwa kwa faragha nchini Uhispania.

 

Dos Santos alikuwa Rais wa Angola kwa karibu miaka 40, hadi mwaka 2017, alifariki dunia Ijumaa, Julai 8, 2022 nchini Hispania.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top