} });
 

Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa akiwa msibani baada ya kuhudhuria mazishi ya vijana waliokufa kwenye klabu nchini mwake.

Rais wa Afrika kusini Cyril Ramaphosa Jumatano alipohudhuria mazishi ya vijana 21 waliofariki kutokana na mkasa kwenye klabu moja ya usiku takriban wiki mbili zilizopita amesema kwamba ni lazima maafisa wan chi hiyo wachukue hatua za kuzuia uuzaji wa pombe kwa vijana walio na umri wa chini.

 

Kwa mujibu wa shirika la habari la AP, Ramaphosa amesema kwamba, ” Huenda tusifahamu hasa kilichotokea, lakini tunachofahamu ni kwamba sheria ilivunjwa usiku huo, na labda mara kadhaa hapo kabla.”

 

Mazishi hayo yanasemekana kuhudhuriwa na zaidi ya waombolezaji 1,000 kwenye mji wa East London wakati majeneza yakipangwa katika mistari miwili.

 

Ramaphosa amehudhuria mazishi hayo wakati taifa lake linapokabiliana na changamoto kadhaa zikiwemo kukatika kwa huduma za umeme, madai ya ufisadi pamoja na uchunguzi unaoendelea wa fedha nyingi zilizopatikana zikiwa zimefichwa kwenye nyumba moja kwenye shamba lake.

soma habari kila siku kazi yetu ni kuhakikisha unapata unachotaka +255 769 305 957 #NURU YA KRISTO INAKUANGAZIA

Facebook Blogger Plugin by TeachMaker

Post a Comment

 
Top